Je, mimi nitawasiliana aje na Baba yangu aliye mbinguni?

 

Ni fursa ya kweli kusema binafsi na Bwana wa mbingu na ardhi wakati wowote!

 

Wanafunzi wa Yesu waliona kiasi cha wakati ambacho Alitumia na Baba yake wa mbinguni. Siku moja waliuliza, 'Unaweza tafadhali tufundishe kuomba?’

 

Jibu lake, mara nyingi huitwa 'Sala ya Bwana,' katika Mathayo 6:9-13. Inalenga juu yake. Huleta kwake mahitaji yetu kwa ajili ya utoaji, msamaha na ulinzi, na kuishia na sifa.

 

Zungumza na Yesu kama rafiki yako bora. Anza kumshukuru na kumsifu kwa upendo wake mkuu kwako. Kisha mwambie matatizo yako. Unaweza kushiriki kitu chochote pamoja naye. Yeye tayari anajua, kwa hivyo usiwe na wasiwasi ati utamshtua.

 

Mingi ya zaburi ya Daudi ni kilio cha msaada katika nyakati za taabu. Katika Zaburi 17, 28, 61, 64, 70 na 86, David anamuita Bwana amsikie na kumlinda.

 

Wakati unajua kuwa umemhuzunisha Bwana, kuja kwake mara moja na kuomba msamaha. Atakusameheni, kukuhamasisha, kukuimarisha na kukuleta kwa uwazi wa matatizo yako.

 

Kumbuka, sala ni mazungumzo ya daima kwa moja ambaye   unajifunza kupenda na kuamini. Kuangalia tu juu angani na kutabasamu juu yake, au kutoa mkono wako kama kumshika Bwana mara moja unaweza kuleta ukaribu ambayo unahitaji.

 

Mstari wa ufunguo

'Msijisumbue kwa kitu, lakini katika kila kitu kwa sala ... pamoja na kushukuru, basi fanya maombi yako yajulikane na Mungu'

Wafilipi 4:6