Ni nini maana ya kufanya upya mawazo yangu?
Kama halijatokea tayari, utapata unakabiliwa na mawazo mabaya. Mimi najua. Ingawa Nimetembea na Kristo kwa miaka mingi, bado kuna mara ambapo mimi humenyana na mitizamo kama ubinafsi, kiburi na ukosefu wa uaminifu.
Tuna bahati kuwa Yesu Kristo hutusaidia kubadili mawazo ya maisha yetu. Hiyo haimaanishi kuwa ni rahisi, lakini inawezekana. Mtume Paulo anaelezea mchakato wa mabadiliko ya njia hivi 'Msiifuatishe namna ya dunia hii, bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu' - Warumi 12 2.
Mungu hataki uweke akili yako kando wakati unakuja kwake. Bali ni kinyume chake. Ameiumba akili yako na anataka uitumie kikamilifu, lakini katika njia sahihi. Anataka iwe upya. Usiwache kufikiri, lakini anza kufikiria na kuangalia mambo kwa mtazamo wake.
Njia kuu ya kuanza ni kutafakari juu ya maandiko. Chukua mistari zilizotajwa katika masomo haya, uyafikirie, hata kuyakariri. Kukariri maandiko huwa ni njia ya nguvu zaidi ya nidhamu na kufanya upya akili yako. Kwa nini usianze sasa hivi? Mstari wa muhimu wa leo (chini) ni wa ajabu wa 'akili-kufanywa upya' katika maandiko. Irudie mara nyingi, na kuifanya rafiki yako katika siku hii.
Mstari wa ufunguo
'Mambo yoyote yaliyo kweli, yoyote yaliyo ya heshima, yaliyo ya haki, yoyote yaliyo safi, yoyote ya kupendeza, yoyote yenye sifa njema, kama kuna wema yoyoote na kama kuna kitu chochote cha sifa - fakaria juu ya mambo haya'
Wafilipi 4:8