Lini mabadiliko mazuri yataanza?

 

Wakati sisi tunafanya aina yoyote ya marekebisho muhimu katika maisha yetu, siku 30 za kwanza ni muhimu. Mafunzo yanaonyesha inachukua hii muda kumwaga tabia ya zamani, au kuanzisha tabia ingine nzuri. Kwa hivyo basi wacha 'tabia' ya kusoma neno la Mungu, tabia yake na njia yake iwe na mizizi ndani yako. Umeanza njia ya maisha, lakini kuna hatari.

 

Hii ni njia mbili ambayo unaweza kupotezwa na jinsi ya kukabiliana na kila mmoja.

 

  • Familia na marafiki ambao hawaelewi. Bila kujali ni kiasi gani au jinsi kidogo umesema kwa wengine, wataona taarifa tofauti kwako. Baadhi yao watataka kujua zaidi, lakini wengine wanaweza kuwa na maadui na maskhara nawe. Bila shaka ni bora si usijihami au kubishana, lakini basi wacha Kristo, ambaye sasa anaishi ndani yako, awapende wao kupitia kwako. Kwa imani, katika muda, wao watataka kubadilika pia. Lakini kila ufanyalo, usiwache wengine wakuvute wewe nyuma katika njia yako ya zamani.
  • Tabia mbaya ambayo haziwezi kuvunjwa kwa urahisi. Labda uko katika uhusiano mbaya au imezidiwa na mapambano ya maisha. Unaweza kujisikia ni vigumu sana. Unaweza kufikiri, 'Siwezi shinda katika maisha mapya.' Je, usiwache mawazo haya yakukumbaie. Kulingana na nilivyoona maishani mwangu, itakuwa si muda mrefu kabla ya kuona baadhi ya ushindi halisi. Kumbuka, Yesu alikuchukua wewe uje kwake mwenyewe tu kama vile ulikuwa. Anakupenda bila masharti na atakuongoza na kukuimarisha kila hatua ya njia.

 

Mstari wa ufunguo

'Yeye aliye ndani yenu ni mkuu kuliko yeye aliye katika dunia'

1 Yohana 4:4