Jinsi gani naweza kuwa na uhakika wa upendo wa Mungu?
Billy Graham, mwinjili mkubwa, alisema, 'ninaposoma Biblia zaidi, ninatambua kwamba Upendo ni uso kuu ya Mungu.'
Nimepata wakati mwingine, kama wewe, ambapo najihisi kuwa mbali na upendo wa Mungu. Labda ulikua katika familia ambayo haikuwa na amani na upendo kidogo au bila upendo kutoka kwa wazazi wako. Unaweza kuwa umepoteza wapendwa wako kwa ugonjwa, ajali au vita. Unaweza kuwa umekabiliwa na umaskini na njaa kama hali halisi ya kila siku. Maumivu maishani mwako hayaishi. Upendo wa Mungu uko wapi kwa haya yote?
Naamini moyo wa Mungu huumwa zaidi ya vile tunaweza jua kwa mateso, udhalimu na mizigo nzito ambayo watoto wake wanapata. Dhambi, wakati iliingia ulimwenguni, ilileta matokeo yanayoathiri maisha yetu ya kila siku.
Lakini upendo wa Mungu aliuonyesha vikuu wakati alimtuma mwana wake, Yesu, kutununua sisi, au 'kutukomboa sisi’, kutoka madhara ya dhambi. Injili ya Yohana anatuambia 'Mungu aliupenda ulimwengu, akamtoa Mwana wake mmoja tu, ndiyo kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele' - Yohana 3:16.
Wakati alipopea maisha yako kwa Mungu, ulikuja uso kwa uso na upendo wa Baba yako wa mbinguni. Sasa, ukiendelea na safari yako, mtegemee kabisa. Mungu anakupenda!
Mstari wa ufunguo
'[Naomba] mjue upendo wa Kristo, ambao hupita elimu yenu, ili mjazwe kabisa utimilifu wote wa Mungu'
Waefeso 3:19