Naweza kutarajia nini katika safari yangu?

 

'Baba tumefika?' Hilo ni swali watoto wetu walikuwa wakiuliza wakati wao walikuwa wadogo, kama tunaenda katika safari ndefu na gari. Niilikuwa nawaeleza kuwa kuna masaa mengi mbele lakini pia wawe na subira na kufurahia safari. 

 

Safari yako ya imani ni zaidi kuliko safari ya gari. Ni mafunzo ya maisha. Kwa kukusaidia njiani. 

 

- Kuwa na uhakika kwamba, chochote ambaco utakutana nacho, Kristo ako na wewe. Aliahidi 'Sitakuacha kamwe, wala sitakutupa' - Waebrania 13 5.

- Angalia mabadiliko madogo, si matokeo ya papo. Baadhi ya mifano ni kukutana rafiki mpya wa Kikristo; kufanya maendeleo kuelekea kushinda tabia mbaya ambayo inakusumbua; kugundua aya ya andiko linakuja hai kwa maisha yako.

 - Kukumbatia kila wakati, kumwamini Mungu kwa siku zijazo.

 

Mabadiliko si rahisi. Tunahitaji kuwa na ukali kwetu sisi wenyewe, hasa wakati tunapotaka kutupa mikono na kuacha njia hii ya Mungu. Lakini kwa kila ushindi, hata iwe ndogo, unatuweka tuwe bora na kupata uwezo wa kupatana na changamoto ijayo.

 

Mara nyingi nimeona maisha ya Kikristo ilikuwa ngumu sana. Tabia za zamani na marafiki ambao walikuwa na ushawishi maskini waliweza kuniteka mimi kama chuma na sumaku. Wakati mwingine mimi nilifanya yale walitaka. Utakuwa na nyakati hizi. Lakini Namshukuru Mungu kuwa sisi si hatujitegemei wenyewe. Tunaweza kumwamini Bwana Yesu, Yule anayeishi ndani yetu kuwa atabaki na sisi kabisa mpaka aone kuwa tumefika njia ya mwisho kwa safari ya maisha.

 

Mstari wa Kusoma

 

'Yeye aliyeanza kazi nzuri ndani yako anawezakuikamilisha hata mpaka siku ya kurudi kwa Yesu Kristo

Wafilipi 1:6